ACETOPHENONE ICSC: 1156
Oktoba 1994

1-Phenylethanone
Phenyl methyl ketone
Acetylbenzene
CAS # 98-86-2 C8H8O / C6H5COCH3
RTECS # AM5250000 Masi ya molekuli: 120.1
UN #
EC # 606-042-00-1
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto.
Povu linalokinza alkoholi, poda kavu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 82°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 82°C, uingizaji hewa.

MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!

Kuvuta pumzi Kuumwa kichwa. Kizunguzungu. Kusinzia.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Ngozi kavu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Kichefuchefu. (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio A/P2 cha mvuke kikaboni na vumbi linalodhuru).
Ainisho ya EU
Alama: Xn
R: 22-36
S: (2-)-26
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Msimbo wa NFPA: H 1; F 2; R 0;
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ACETOPHENONE ICSC: 1156
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI AU FUWELE NYEUPE YENYE HARUFU TAMBULISHI.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 10 ppm; 49 mg/m³ (ACGIH 1993-1994)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C wakati wa kunyunyiza au kutawanya, hata hivyo, kwa kasi zaidi.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kusababisha kupoteza fahamu.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Kioevu hukausha ngozi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 202°C
Kiwango myeyuko: 20°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.03
Umumunyifu katika maji: mbaya
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 15°C: 0.133
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.1
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1
Kiwango cha kumweka: 82°C o.c.
Jotoridi la kujiwasha: 571°C
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.58
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Hypnone ni jina la kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005