| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua sana.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Poda, povu linalokinza alkoholi, maji mengi, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kizunguzungu. Kusinzia. Kuumwa kichwa. Kuumwa koo. Kupoteza fahamu.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Ngozi kavu. Wekundu. Maumivu. (Tazama Kuvuta pumzi).
|
Glavu za kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Miwani ya usalama.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Maumivu ya tumbo. Kichefuchefu. Kutapika. (Tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Kisichoingiza hewa. Ainisho ya EU Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 3 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 674 Msimbo wa NFPA: H 2; F 3; R 2; |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Baridi. Weka gizani. Kilichofungwa vizuri. Hifadhi iwapo tu imetulia.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI VUKIVU MNO CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii huenda ikatengeneza peroksidi lipukaji. Huweza kulipuka wakati wa kukanza. Humenyuka kwa nguvu ikiwa na vioksidishaji vikali kusababisha athari ya moto na mlipuko. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 1000 ppm; 3110 mg/m³ (ACGIH 1991-1992) |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kupitia kwenye ngozi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Mfiduo juu zaidi ya OEL huweza kusababisha kupoteza fahamu. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Kioevu hukausha ngozi. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 42°C Kiwango myeyuko: -105°C Uzito wiani (maji = 1): 0.86 Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 33 Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 44 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.6 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.7 Kiwango cha kumweka: -18°C o.c. Jotoridi la kujiwasha: 237°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.6-17.6 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Ongezeko la kiimarishaji au kiviza huweza kuathiri tabia ya kitoksini za dutu hii, shauriana na mtaalam. Kagua kama kuna peroksidi kabla ya kunereka; iwapo chanya fanya iwe salama. Methilali hugeuzwa kuwa methanoli na fomaldehidi na yaweza kuonyesha athari kama ile. Ona ICSC 0057 Methanol na 0275 Formaldehyde.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||