n-BUTYL ETHER ICSC: 1150
Aprili 1994

Di-n-butyl ether
1,1'-Oxybis(butane)
1-Butoxybutane
CAS # 142-96-1 C8H18O / (CH3(CH2)3)O
RTECS # EK5425000 Masi ya molekuli: 130.2
UN # 1149
EC # 603-054-00-9
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na nyuso za moto.
AFFF, povu linalokinza alkoholi, poda kavu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 25°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 25°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza).
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kusinzia. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Ngozi kavu. Wekundu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Mchomo. Kichefuchefu. Kuumwa koo.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio A/P2 cha mvuke kikaboni na vumbi linalodhuru).
Kisichoingiza hewa.
Ainisho ya EU
Alama: Xi
R: 10-36/37/38
S: (2-)
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 584
Msimbo wa NFPA: H 2; F 3; R 0;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na maunzi yasiokubaliana. Tazama Hatari za Kikemikali. Baridi. Weka gizani. Hifadhi iwapo tu imetulia.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
n-BUTYL ETHER ICSC: 1150
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI

HATARI KWA MWILI:
Kutokana na mtiririko, mchukucho n.k., chaji za kiumemetuamo huweza kutokea.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii huweza kutengeneza peroksidi lipukaji, hasa aina isiyo na maji. Humenyuka ikiwa na vioksidishaji. Humenyuka vikali ikiwa na trikloridi nitrojeni (NCl_3).

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva na ini.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Kioevu hukausha ngozi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 142°C
Kiwango myeyuko: -95°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.8
Umumunyifu katika maji: hakuna (<0.1 g/100 ml)
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.64
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.5
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.0
Kiwango cha kumweka: 25°C
Jotoridi la kujiwasha: 194°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.5-7.6
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.08 (calc)
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa viumbe hai vya majini.
VIDOKEZO
Ongezeko la kiimarishaji au kiviza huweza kuathiri tabia ya kitoksini za dutu hii, shauriana na mtaalam. Kagua kama kuna peroksidi kabla ya kunereka; iwapo chanya fanya iwe salama.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005