TETRASODIUM PYROPHOSPHATE ICSC: 1140
Aprili 1997

Sodium pyrophosphate
Pyrophosphoric acid, tetrasodium salt
CAS # 7722-88-5 Na4O7P2
RTECS # UX7350000 Masi ya molekuli: 266
UN #
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa (iwapo si poda).
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Kichefuchefu. Kutapika. Kuhara.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Osha salio kwa maji mengi. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P1 cha chembe ajizi).
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI


IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
TETRASODIUM PYROPHOSPHATE ICSC: 1140
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA AU FUWELE ISO RANGI AU NYEUPE, ISO HARUFU

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa. Mmumunyo huu katika maji ni besi dhaifu.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 5 mg/m³ (ACGIH 1996)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi yenye vumbi hili na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka iwapo katika hali ya poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 988°C (ona Vidokezo)
Uzito wiani (maji = 1): 2.5
Umumunyifu katika maji: wastani (6.7 g/100ml ifikapo 25°C)
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Viwango myeyuko vinginevyo: 880°C (poda).
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005