| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usigusishe na vinavyoweza kuwaka.
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na dutu za kuwaka na vinakisishaji.
|
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kuumwa koo. Kufanyiza kisauti wakati wa kupumua.
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu. Maumivu.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Kuhara. Kichefuchefu. Kuumwa koo. Kutapika.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo. Kusanya salio kwa uangalifu, Kisha osha kwa maji mengi. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
|
Ainisho ya EU Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 5.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 51G02-I+II+III
|
Kilichofungwa vizuri. Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi, besi kali, poda ya metali.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: FUWELE AU PODA NYEUPE HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii ni kioksidishaji madhubuti na humenyuka iwapo na maunzi yanayoweza kuwaka na yanayonakisi. Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi pamoja na oksidi za sulfuri. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na poda ya metali na besi kali. Mmumunyo huu katika maji ni asidi dhaifu. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: (kama pasalfeti) 0.1 mg/m³ (ACGIH 2001). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji Kuvuta pumzi yenye vumbi kunaweza kusababisha pumu (tazama Vidokezo). ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Kuvuta hewa kwa kurudia au muda mrefu huweza kusababisha pumu. Yaweza kusbabisha muwasho (general allergic reaction) kama kwa ngozi au kuzimia. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Hutengana chini ya kiwango myeyuko ifikapo 180°C Uzito wiani: 1.1 g/cm³ Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 55.6 |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi. Mtu yeyote aliyeonyesha dalili za pumu kutokana na dutu hii kamwe asigusane na dutu hiyo tena. Aghalabu dalili za pumu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Kwa hiyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||