CALCIUM PHOSPHIDE ICSC: 1126
Machi 2002

CAS # 1305-99-3 Ca3P2
RTECS # EW3870000 Masi ya molekuli: 182.2
UN # 1360
EC # 015-003-00-2
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki lakini hutengeneza gesi inayoungua ikigusana na maji au hewa nyevunyevu.
Usigusishe na maji, vioksidishaji na asidi.
USITUMIE maji au povu. Moto unapotokea katika eneo: poda, dioksidi kaboni.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza mapipa n.k. kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kuumwa koo. Kupumua kwa shida. Tetemeko. Kuhara. Degedege. Kutapika.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Mpeleke kwa matibabu. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Huduma ya kusaidia kupumua ya mdomo kwa mdomo hairuhusiwi.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Mavazi ya kinga. Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Mpeleke kwa daktari. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Huduma ya kusaidia kupumua ya mdomo kwa mdomo hairuhusiwi.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Ainisho ya EU
Alama: T+, F, N
R: 15/29-28-50
S: (1/2-)-22-43-45-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 4.3
Jasara tanzu za UN: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 43GWT2-I
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho na maunzi yasiokubaliana. Tazama Hatari za Kikemikali. Baridi. Kavu. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
CALCIUM PHOSPHIDE ICSC: 1126
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA FUWELE NYEKUNDU-KAHAWIA AU MABONGE KIJIVU.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka kwa ukali sana pamoja na asidi, maji au hewa yenye unyevunyevu kusababisha fosfini (ICSC 0694), kusababisha athari ya moto na yenye sumu. Humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji vikali kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Kikolezo cha chembechembe cha sumu sana yaweza kufikiwa haraka ikitawanywa hasa kama poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi yenye fosfini kutoka kwa fosfidi kalsiamu kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Dutu hii huweza kuathiri njia ya utumbo, mfumo mkuu wa neva, ini, mafigo na mfumo wa moyo na mishipa kusababisha kuharibika kwa utendaji na kutoweza kupumua. Mfiduo huweza kusababisha kifo.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 1600°C
Uzito wiani: 2.5 g/cm³
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Photophor ni jina la kibiashara. Madhara kwa mazingira ya mkabala na dutu hii hayajachunguzwa vya kutosha. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005