SODIUM CHLORATE ICSC: 1117
Oktoba 1999

Chloric acid, sodium salt
CAS # 7775-09-9 NaClO3
RTECS # FO0525000 Masi ya molekuli: 106.44
UN # 1495
EC # 017-005-00-9
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usigusishe na dutu ziwakazo. Usigusishe na vinavyoweza kuwaka vinakisishaji na maunzi kikaboni.
Maji mengi.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko.

Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo. Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Kuchanganyikiwa. Degedege. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kupoteza fahamu.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga.
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kukosa pumzi. Kutapika. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
Ainisho ya EU
Alama: O, Xn
R: 9-22
S: (2-)-13-17-46
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 5.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 47/51G02
Msimbo wa NFPA : H 1; F 0; R 2; OX
Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi, na maunzi yasiokubaliana. Tazama Hatari za Kikemikali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
SODIUM CHLORATE ICSC: 1117
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
CHEMBECHEMBE AU FUWELE ISO RANGI ISO HARUFU

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa zaidi ya 300°C huzalisha oksijeni, ambayo huongeneza athari ya moto, na mafusho yenye sumu (klorini). Dutu hii ni kioksidishaji madhubuti na humenyuka kwa ukali sana iwapo na maunzi yanayoweza kuwaka na yanayonakisi, kusababisha athari ya moto na mlipuko. Humenyuka pamoja na misombo kikaboni mingi kutoa michanganyiko isiyohimili mshtuko kusababisha athari ya mlipuko. Hushambulia zinki na chuma.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka wakati wa kunyunyiza au inapotawanywa hasa iwapo katika hali ya poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri damu, kusababisha kufanyika kwa methemoglobini, na mafigo, kusababisha kuharibika kwa figo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Tazama Vidokezo.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Hutengana chini ya kiwango mchemko ifikapo takribani 300°C
Kiwango myeyuko: 248°C
Uzito wiani: 2.5 g/ml
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 100
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Dutu hii hutengana kabisa inapozidi 300°C. Haitahimili mshtuko ikiingiwa na maunzi kikaboni. Miundo inayouzwa huwa vizuihisi vya moto. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi. Dervan, Defol, Chlorax na Atlacide ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005