PERCHLORYL FLUORIDE ICSC: 1114
Oktoba 1999

Chlorine oxyfluoride
Chlorine fluoride oxide
Trioxychlorofluoride
(silinda)
CAS # 7616-94-6 ClFO3
RTECS # SD1925000 Masi ya molekuli: 102.45
UN # 3083
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
Glavu za kuhami baridi. Mavazi ya kinga.
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
Macho
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.

KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 2.3
Jasara tanzu za UN: 5.1

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20G45
Isodhurika kwa moto iwapo ndani ya jengo.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
PERCHLORYL FLUORIDE ICSC: 1114
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI ISO RANGI AU GESI OEVU ILIYOBANWA, YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii ni kioksidishaji madhubuti na humenyuka kwa ukali sana iwapo na maunzi yanayoweza kuwaka na yanayonakisi, kwa athari ya moto au mlipuko. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na besi za nitrojeni na misombo kikaboni laini kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia aina fulani za plastiki, mpira na mipako.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 3 ppm kama TWA;
6 ppm kama STEL (ACGIH 1999).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi yenye gesi kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Kuvuta pumzi wa viwango vya juu kunaweza kusababisha kufanyika kwa methemoglobini. Kioevu hiki huweza kusababisha jamidi. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Athari zinaweza kuchelewa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri damu, kusababisha kufanyika kwa methemoglobini. Dutu hii yaweza kusababisha mabadiliko kwa mifupa kwa sababu ya florini (fluorosis). (Tazama Vidokezo).
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: -46.7°C
Kiwango myeyuko: -147.7°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.4 (kioevu)
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.06
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005