N,N'-ETHYLENE BIS(STEARAMIDE) ICSC: 1112
Aprili 1997

1,2-Bis(octadecanamido)ethane
N,N'-Ethylene distearylamide
N,N'-Ethylene bis(octadecanamide)
CAS # 110-30-5 C38H76N2O2
RTECS # None Masi ya molekuli: 593
UN #
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto.
Mnyunyizio wa maji, povu, poda kavu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.

MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi Kikohozi.
Uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga.
Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu.
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P1 cha chembe ajizi).
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
N,N'-ETHYLENE BIS(STEARAMIDE) ICSC: 1112
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
MANGO KAMA NTA, NYEUPE KATIKA MAUMBO MBALIMBALI

HATARI KWA MWILI:
Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana ifkapo 260°C inapokanzwa na inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu (oksidi za nitrojeni). Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vikali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya vumbi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaokera unaweza kufikiwa haraka ikiwa kama poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera kwa upole macho, ngozi na njia ya upumuaji.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Hutengana chini ya kiwango mchemko ifikapo 260°C
Kiwango myeyuko: 135-146°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.97
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kiwango cha kumweka: 280°C o.c.
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Advawax, Lubrol EA na Microtomic 280 ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005