| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto.
|
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Maumivu ya tumbo. Kichefuchefu. Kutapika. Homa na baridi kali.
|
Uingizaji hewa (hapana kama ni poda), mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
|
Miwani ya usalama, au kingao cha uso.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Manjano ya macho na ngozi. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu). Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari. Ainisho ya EU Alama: T, N R: 45-20/21/22-43-48/20/21-51/53 S: 53-45-61 Angalia: [E] Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 865/61G06 Msimbo wa NFPA : H 3; F 1; R 0; |
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: MAGAMBA ISO RANGI HADI MANJANO ISIYOKOZA, YENYE HARUFU TAMBULISHI. HUGEUKA GIZA INAPOFIDULIWA NA HEWA. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa au inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu kama vile anilini na oksidi za nitrojeni. Dutu ni besi dhaifu. Humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji vikali. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV (kama TWA): 0.1 ppm; 0.81 mg/m³ A3 (ngozi) (ACGIH 1998) |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii huweza kuathiri ini, kusababisha kuharibika kwa ini. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano .unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko ifikapo 102 kPa: 398-399°C Kiwango myeyuko: 91.5-92°C Uzito wiani: 0.5 g/cm³ Umumunyifu katika maji: mbaya Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 197°C: 133 |
Kiwango cha kumweka: 220°C c.c. Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.6 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira kwa sababu hubakia kwenye mazingira.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Ancamine TL, Araldite hardener 972, Epicure DDM, Slumicure M, Tonox ni majina ya kibiashara.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||