2,4-DINITROANILINE ICSC: 1107
Oktoba 1999

2,4-Dinitrobenzenamine
2,4-Dinitrophenylamine
1-Amino-2,4-dinitrobenzene
CAS # 97-02-9 C6H5N3O4 / C6H3(NH2)(NO2)2
RTECS # BX9100000 Masi ya molekuli: 183.1
UN # 1596
EC # 612-040-00-1
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T+, N
R: 26/27/28-33-51/53
S: (1/2-)-28-36/37-45-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 875/61G12
Msimbo wa NFPA : H 3; F 1; R 3;
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
2,4-DINITROANILINE ICSC: 1107
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE MANJANO YENYE UMBO KAMA SINDANO AU VIPANDE VYA KIJANI-NJANO AU MANGO MANJANO, YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Huweza kulipuka wakati wa kukanza au kutokana na msuguano. Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu kama vile oksidi za nitrojeni. Humenyuka ikiwa na vioksidishaji.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri damu, kusababisha kufanyika kwa methemoglobini.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 187-188°C
Uzito wiani: 1.62 g/cm³
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kiwango cha kumweka: 222-224°C c.c.
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.84 (imekadiriwa)
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005