TETRAMETHYLAMMONIUM CHLORIDE ICSC: 1099
Novemba 2003

Ammonium-, tetramethyl-, chloride
N, N, N-Trimethylmethanamium chloride
Tetramine chloride
N, N, N-Trimethylmethanaminium chloride
CAS # 75-57-0 C4H12ClN / (CH3)4NCl
RTECS # BS7700000 Masi ya molekuli: 109.6
UN # 2811
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki.

Moto unapotokea katika eneo: poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO


Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kuumwa koo. Kukosa pumzi.
Uingizaji hewa. Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu. Maumivu. Kiwaa.
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kizunguzungu. Kichefuchefu. Kuumwa koo. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vilivyofunikwa; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Osha salio kwa maji mengi. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT2-II
Kinachotenganishwa na vioksidishaji. Kavu. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
TETRAMETHYLAMMONIUM CHLORIDE ICSC: 1099
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE RISHAI, NYEUPE

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa zaidi ya 300°C huzalisha amonia, monoksidi kaboni, kloridi hidrojeni na oksidi za nitrojeni. Humenyuka pamoja na vioksidishaji.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki. MAK haijathibitishwa.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko (hutengana): 368-370°C
Uzito wiani: 1.17 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: vizuri sana
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Madhara kwa mazingira ya mkabala na dutu hii hayajachunguzwa.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005