1,3-DICHLOROBENZENE ICSC: 1095
Oktoba 2000

m-Dichlorobenzene
m-Phenylene dichloride
CAS # 541-73-1 C6H4Cl2
RTECS # CZ4499000 Masi ya molekuli: 147.00
UN # 2810
EC # 602-067-00-7
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 63°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 63°C, uingizaji hewa.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kusinzia. Kichefuchefu. Kuumwa koo. Kutapika. Tazama Vidokezo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Mchomo. Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio A/P2 cha mvuke kikaboni na vumbi linalodhuru).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: Xn, N
R: 22-51/53
S: (2-)-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, alumini, vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
1,3-DICHLOROBENZENE ICSC: 1095
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu kama vile kloridi hidrojeni. Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vikali. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na alumini.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Mvuke huu inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Tazama Vidokezo.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri mafigo and ini. See Notes.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 173°C
Kiwango myeyuko: -24.8°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.288
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 25°C: 0.286
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 5.1
Kiwango cha kumweka: 63°C
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.53
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini. Kuzidisha kwa kemikali yaweza kutokeakwa samaki.
VIDOKEZO
Data on the toxicity of m-dichlorobenzene are limited. Ona ICSC 0037 (p-Dichlorobenzene) na 1066 (o-Dichlorobenzene).
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005