ETHYL CHLOROACETATE ICSC: 1081
Oktoba 2001

Chloroacetic acid, ethyl ester
Ethyl monochloroacetate
Ethyl alpha-chloroacetate
Ethyl-2-monochloroacetate
CAS # 105-39-5 C4H7ClO2 / ClCH2CO2C2H5
RTECS # AF9110000 Masi ya molekuli: 122,55
UN # 1181
EC # 607-070-007
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda kavu, mnyunyizio wa maji, povu linalokinza alkoholi, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 53°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 53°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa n.k. kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Inayotoza machozi. Wekundu. Maumivu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Mchomo ya ulimi. Kichefuchefu. Maumivu ya tumbo. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vya plastiki vyenye mifuniko. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga mkavu au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 23/24/25-50
S: (1/2-)-7/9-45-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Jasara tanzu za UN: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61S1181
Msimbo wa NFPA: H ; F 3; R 0;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na maunzi yasiokubaliana, vyakula na malisho. Tazama Hatari za Kikemikali. Kavu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ETHYL CHLOROACETATE ICSC: 1081
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU KALI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha gesi zenye sumu na babuzi kama vile kloridi hidrojeni na mafusho ya asidi asetiki. Humenyuka pamoja na maji, hewa yenye unyevunyevu na asidi kusababisha kloridi hidrojeni (tazama ICSC 0163). Humenyuka pamoja na besi, vioksidishaji na kinakisishaji.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
MAK haijathibitishwa.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera kwa ukali macho, na inakera kwa kiasi ngozi na njia ya upumuaji.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 144.2°C
Kiwango myeyuko: -26°C
Uzito wiani: 1.15 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 1.23
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 450
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.2
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.01
Kiwango cha kumweka: 53°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 452°C
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.28 (imekadiriwa)
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Vikomo vya ulipukaji havijulikani katika maandiko, japokuwa dutu hii inaweza kuwaka na ina kiwango cha kumweka pungufu ya 61°C.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005