| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka.
|
Usiwashe moto.
|
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Ngozi kugeuka kuwa bluu. Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kukosa pumzi. Kuchanganyikiwa. Degedege. Kupoteza fahamu. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu. Tazama Vidokezo.
|
| Ngozi |
Wekundu.
|
Glavu za kinga.
|
Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
|
| Macho |
|
Miwani ya usalama.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
(Tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Kupumzika. Mpeleke kwa daktari. Tazama Vidokezo.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru). Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari. Ainisho ya EU Alama: Xn, N R: 22-51/53 S: (2-)-22-24-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G12c
|
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: FUWELE MANJANO YENYE UMBO KAMA SINDANO HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha gesi zenye sumu na babuzi, kama vile oksidi za nitrojeni. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki. MAK haijathibitishwa. |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera kwa upole ngozi. Dutu hii huweza kuathiri damukusababisha kufanyika kwa methemoglobini. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Athari zinaweza kuchelewa. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: >200°C Kiwango myeyuko: 108°C Uzito wiani: <1 g/cm³ Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: hakuna Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 25°C: 0.00046 |
Kiwango cha kumweka: 205°C Jotoridi la kujiwasha: 522°C Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.3 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kusababisha madhara yatakayoonekana baadaye katika mazingira ya maji.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||