BROMOACETONE ICSC: 1074
Aprili 2005

Bromo-2-propanone
Acetyl methyl bromide
CAS # 598-31-2 C3H5BrO
RTECS # UC0525000 Masi ya molekuli: 137.0
UN # 1569
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Mnyunyizo wa maji, poda.
MLIPUKO


MFIDUO


Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kuumwa koo. Kupumua kwa shida.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Kutoa machozi. Wekundu. Maumivu. Kiwaa.
Miwanivuli ya usalama, au au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Mchomo kooni na kifuani. Kikohozi. Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Osha salio kwa maji mengi.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Jasara tanzu za UN: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GTF1-II
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali,, vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
BROMOACETONE ICSC: 1074
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI. HUGEUKA URUJUANI INAPOFIDULIWA NA MWANGA.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa kuzalisha mafusho yenye sumu pamoja na bromidi hidrojeni. Humenyuka ikiwa na vioksidishaji.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki. MAK haijathibitishwa.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Inayotoza machozi. Dutu hii inakera kwa ukali macho, ngozi na njia ya upumuaji.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Tazama Vidokezo.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 137°C
Kiwango myeyuko: -36.5°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.63
Umumunyifu katika maji: mbaya
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 1.1
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.04
Kiwango cha kumweka: 51.1°C
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.11
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Madhara ya afya yatokanayo na kuingia mwilini dutu hii hayajachunguzwa vya kutosha.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005