o-CHLOROBENZYLIDENEMALONONITRILE ICSC: 1065
Oktoba 2002

[2-(Chlorophenyl)methylene]malononitrile
2-Chlorobenzylidene malononitrile
(o-Chlorobenzal)malononitrile
beta,beta-Dicyano-o-chlorostyrene
[(2-Chlorophenyl)methylene]propanedinitrile
CS (riot control agent)
CAS # 2698-41-1 C10H5ClN2 / ClC6H4CH=C(CN)2
RTECS # OO3675000 Masi ya molekuli: 188.6
UN # 3276
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.

MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kichefuchefu. Kuumwa koo. Kutapika.
Mtambo wa kutolea nje.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi Wekundu. Mchomo. Maumivu. Malengelenge.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Inayotoza machozi. Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kingao cha uso.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Mchomo kooni na kifuani.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Vuta kiombwe maunzi yaliyomwagika. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT1-III
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
o-CHLOROBENZYLIDENEMALONONITRILE ICSC: 1065
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA FUWELE NYEUPE YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka kwa ukali sana pamoja na besi kali na asidi kuzalisha amonia. Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu pamoja na kloridi hidrojeni, sianidi hidrojeni na oksidi za nitrojeni. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.05 ppm (Kiwango cha juu); (ngozi); A4; (ACGIH 2002).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka wakati wa kunyunyiza au inapotawanywa hasa iwapo katika hali ya poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Inayotoza machozi. Dutu hii inakera kwa ukali macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mapafu.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 310-315°C
Kiwango myeyuko: 93-96°C
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.1-0.5
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo °C: 0.0045
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 6.5
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Kikomo thamani cha mfiduo matumizi ya kazi kisivukwe wakati wowote wa mfiduo amilifu.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005