| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kuumwa koo. Mchomo. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Mibabuko ya ngozi. Maumivu. Wekundu.
|
Glavu za kinga.
|
Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Maumivu. Wekundu. Kuungua kunakopenya sana.
|
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Maumivu ya tumbo. Mchomo kooni na kifuani. Kuumwa koo. Kichefuchefu. Kutapika. Mshtuko au kuzimia.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu). Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: C, N R: 34-50/53 S: (1/2-)-7/8-28-45-60-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 8 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 80GC2-II+III
|
Kinachotenganishwa na besi kali, vyakula na malisho. Kavu. Kilichofungwa vizuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: MANGO YA RISHAI NYEUPE KATIKA MAUMBO MBALIMBALI HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu ya kloridi hidrojeni na oksidi zinki. Mmumunyo huu katika maji ni asidi kali ya kati. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV (kama mafusho): 1 mg/m³ (kama TWA) (ACGIH 2001) TLV (kama mafusho): 2 mg/m³ (kama STEL) (ACGIH 2001) |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa hasa iwapo katika hali ya poda. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho na ngozi. Erosoli hii inakera njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Kuvuta pumzi mafusho kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Dutu hii huweza kuathiri kongosho, ikimeswa. Mfiduo kwa kiasi kikubwa cha mvuke wa kloridi ya zinki yaweza kusababisha kushindwa kupumua (Adult Respiratory Distress Syndrome), na ufumwele kwa mapafu na kifo. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 732°C Kiwango myeyuko: 290°C Uzito wiani: 2.9 g/cm³ Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 432 vizuri sana |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Nambari nyngine za UN: 1840 Zinc chloride, mmumunyo kwenye maji, ainisho ya hatari 8. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||