| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Povu, poda kavu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 30°C.
|
Mfumo funge wa zaidi ya 30°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza). Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kuchanganyikiwa. Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kuumwa koo. Kukosa pumzi.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu. Maumivu.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
|
| Macho |
Kiwaa. Maumivu. Wekundu.
|
Miwani ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Mchomo. Maumivu ya tumbo. Kichefuchefu. Kutapika. Kuchanganyikiwa. Degedege. Kuhara. Kupoteza fahamu.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Funika dutu iliyomwagika kwa udongo, mchanga mkavu au au nyenzo isiyochomeka. Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo na kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu). Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
|
Kichafuzi cha maji/bahari. Ainisho ya EU Alama: Xn, N R: 10-20/21/22-36/38-43-51/53-65 S: (2-)-36/37-46-61-62 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 3 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S1299 Msimbo wa NFPA: H 1; F 3; R 0; |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, maunzi yasiokubaliana. Tazama Hatari za Kikemikali. Baridi. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI ZA KIKEMIKALI: Inapowaka hutengeneza mafusho yenye sumu -kama vile monoksidi kaboni. Dutu hii hutengana polepole inapoathiriwa na hewa au mwanga huzalisha matokeo ya uoksidishaji wenye sumu kuliko terafini yenewe. Humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji, halojeni, dutu zinazoweza kuwaka, asidi minerali. Hushambulia plastiki na mpira. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 100 ppm (kama TWA); SEN Kusudio kubadili; (ACGIH 2001). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Mvuke huu inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kumeza kioevu hiki kunaweza kusababisha madhara kwenye mapafu kukifyonza na kunaweza kuleta kichomi kinachotokana na kemikali. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, kibofu na mafigo kusababisha ukereketwaji, degedege na kuharibika kwa figo. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kusababisha moyo kwenda haraka (tachycardia), kupoteza fahamu, matatizo ya kupumua, kifo. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Kioevu hukausha ngozi. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 149 hadi 180°C Kiwango myeyuko: -50 hadi -60°C Uzito wiani (maji = 1): 0.9 Umumunyifu katika maji: hakuna Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.25 hadi 0.67 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.6 hadi 4.8 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.01 Kiwango cha kumweka: 30 hadi 46°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 220 hadi 255°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 0.8-6 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kusababisha madhara yatakayoonekana baadaye katika mazingira ya maji.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Terafini hupatikana kwa kutonesha sandaruki kutoka kwa msonobari tofauti ni mchanganyiko wa hidrokaboni (terpene). Asili hutegemea njia ya kutonesha, umri, mahali na aina ya mti inayotoka.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||