ETHYLENE GLYCOL DINITRATE ICSC: 1056
Oktoba 1999

Glycol dinitrate
EGDN
Nitroglycol
CAS # 628-96-6 C2H4N2O6 / NO2-OCH2CH2O-NO2
RTECS # KW5600000 Masi ya molekuli: 152.1
UN #
EC # 603-032-00-9
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Kilipukaji. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni. Ondoa watu wote na uzime moto kutoka mahali inayostahimili mlipuko.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko.
Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza). Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche. USIACHE kikaathiriwa na msuguano au mshtuko.
Utokeapo moto: poza mapipa n.k. kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Kuumwa kichwa. Kizunguzungu. Kichefuchefu. Udhaifu. Kujisikia joto na kujaa usoni. Maumivu kifuani. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! (Tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: E, T+
R: 2-26/27/28-33
S: (1/2-)-33-35-36/37-45
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Isodhurika kwa moto. Hifadhi kwenye jengo lililotengwa. Kinachotenganishwa na asidi, vyakula na malisho. Baridi. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ETHYLENE GLYCOL DINITRATE ICSC: 1056
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI HADI MANJANO, KAMA MAFUTA

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Kukanza kunaweza kusababisha mwako au mlipuko mkali kutoa mafusho yenye sumu (oksidi za nitrojeni). Huweza kutengana kwa mlipuko kutokana na mshtuko, msuguano, mtikiso. Humenyuka pamoja na asidi.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.05 ppm; (as TWA) (ngozi) (ACGIH 1999)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa moyo na mishipa, kusababisha nguvu ya damu kupungua kwa kasi. Dutu hii huweza kuathiri damu, kusababisha kufanyika kwa methemoglobini. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Athari zinaweza kuchelewa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Kuwa nayo kila mara huleta mazoea. Lakini kusiokuwako kwa muda mfupi yaweza kusababisha kifo kwa ghafula.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: hulipuka ifikapo 114°C
Kiwango myeyuko: -22°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.49
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 0.5
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 7
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 5.2
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.0
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.16
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Dalili kama kuumwa kifua, kupiga moyo kwa nguvu inayojia wakati hauko kwa kazi ni dalili ya kiwango cha sumu ya dutu hii na lazima ijulishwe kwa daktari anayehusika. Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005