| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki. Ukanzaji unaweza kusababisha ongezeko la kanieneo na kuleta athari ya kupasuka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
|
|
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji.
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kuumwa koo. Kusinzia. Kuchanganyikiwa. Kichefuchefu. Kutapika. Kikohozi. Kupoteza fahamu. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI. KIOEVU YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Maumivu.
|
Glavu za kuhami baridi. Mavazi ya kinga.
|
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI. Wekundu. Maumivu.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. Ondoa mvuke kwa mnyunyuzio mwembamba wa maji. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
|
Kichafuzi cha maji/bahari. Ainisho ya EU Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 2.3 Jasara tanzu za UN: 8 | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 801
|
Isodhurika kwa moto iwapo ndani ya jengo. Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Baridi.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: GESI OEVU ILIYOBANWA ISO RANGI, YENYE HARUFU KALI. HATARI KWA MWILI: Gesi hii ni nzito kuliko hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi (sianidi hidrojeni, kloridi hidrojeni, oksidi za nitrojeni) Humenyuka taratibu pamoja na maji au mvuke ya maji kutoa kloridi hidrojeni. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 0.3 ppm; kama (viwango vya juu kabisa) (ACGIH 1999). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Inayotoza machozi. Dutu hii inakera sana macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri respiresheni ya seli, kusababisha degedege and kuzirai, kupoteza fahamu. Mfiduo huweza kusababisha kifo. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Tazama Vidokezo. Kuvuta pumzi yeney dutu hii kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Athari zinaweza kuchelewa. Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 13.8°C Kiwango myeyuko: -6°C Umumunyifu katika maji: humumunyika Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 21.1°C: 1987 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.16 |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kikomo thamani cha mfiduo matumizi ya kazi kisivukwe wakati wowote wa mfiduo amilifu. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya mnyunyuzio mwafaka unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Usinyunyizie maji juu ya silinda inayovuja (kuzuia ulikaji wa silinda). Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||