AMMONIUM CHLORIDE ICSC: 1051
Aprili 2000

Sal ammoniac
CAS # 12125-02-9 NH4Cl
RTECS # BP4550000 Masi ya molekuli: 53.5
UN #
EC # 017-014-00-8
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO


Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa (hapana kama ni poda), mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Kichefuchefu. Kuumwa koo. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Osha salio kwa maji mengi. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
Ainisho ya EU
Alama: Xn
R: 22-36
S: (2-)-22
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Msimbo wa NFPA : H 1; F 0; R 0;
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 90G02
Kinachotenganishwa na nitrati amonia, kloreti potasiamu. Kavu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
AMMONIUM CHLORIDE ICSC: 1051
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
MANGO KATIKA MAUMBO MBALIMBALI, ISO HARUFU, ISO RANGI HADI NYEUPE, YA RISHAI

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi (oksidi za nitrojeni, amonia na hidrojeni chloride). Mmumunyo huu katika maji ni asidi dhaifu. Humenyuka vikali ikiwa na nitrati amonia na kloreti potasiamu kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia shaba na vitu vitokanavyo na shaba.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (kama vumbi): 10 mg/m³ (kama TWA);
20 mg/m³ (kama STEL) (ACGIH 1998).
MAK haifahamiki
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi yenye vumbi au mafusho na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaokera unaweza kufikiwa haraka.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 520°C
Kiwango myeyuko (hutengana): 338°C
Uzito wiani: 1.5 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 28.3
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 160°C: 0.13
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO

MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005