| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na asidi, vioksidishaji.
|
Maji mengi, mnyunyizio wa maji, povu, poda kavu.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Mchomo. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi. Kuumwa koo.
|
Mfumo funge na uingizaji hewa.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu. Maumivu. Mibabuko ya ngozi. Malengelenge.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kiwaa. Kuungua kunakopenya sana.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Maumivu ya tumbo. Mchomo. Mshtuko au kuzimia.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoa vyanzo vyote vya moto. Funika dutu iliyomwagika kwa udongo au mchanga mkavu. Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
|
Kisichoingiza hewa. Ainisho ya EU Alama: C, N R: 31-34-50 S: (1/2-)-26-45-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 4.2 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Msimbo wa NFPA: H 3; F 1; R 1;
|
Kinachotenganishwa na asidi, vioksidishaji. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri. Kavu.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: FUWELE NYEUPE HADI MANJANO, RISHAI YENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapochomwa inapogusana na asidi, maji, huzalisha gesi babuzi na zenye sumu, ambayo huongeza athari ya moto. Mmumunyo huu katika maji ni besi kali, humenyuka vikali ikiwa na asidi na husabisha ulikaji. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki. |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kupitia katika ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Kikolezo cha chembechembe ya dhuru yaweza kufikiwa haraka ikitawanywa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango myeyuko (hutengana): 920-950°C Uzito wiani: 1.86 g/cm³ |
Jotoridi la kujiwasha: > 480°C Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -3.5 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa viumbe hai vya majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Nambari nyingine za UN: 1849, sulfidi sodiamu, mmumunyo wa maji 30% au zaidi ya 30%, ainisho ya hatari 8, kikufundi ufungashaji cha UN II. Viwango myeyuko vinginevyo: 1180°C bila hewa.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||