| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua sana.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Mnyunyizio wa maji, povu linalokinza alkoholi, poda kavu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 24°C.
|
Mfumo funge wa zaidi ya 24°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
|
|
| Kuvuta pumzi |
Mchomo. Kikohozi. Kukosa pumzi. Zaidi (tazama Kumeza).
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu. Maumivu.
|
Glavu za kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Miwani ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Mchomo kooni na kifuani. Kichefuchefu. Kutapika. Kuhara. Kusinzia. Kupoteza fahamu.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo visivyo vya plastiki vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni).
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: F R: 11 S: (2-)-9-16-29-33 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 3 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S1264 Msimbo wa NFPA: H 2; F 3; R 1; |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho, besi na vioksidishaji.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana kwa kisimama inapoathiriwa na hewa na mwanga. Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu. Humenyuka pamoja na besi na vioksidishaji. Hushambulia plastiki. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki. |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa neva kusababisha kuizoea. Dutu hii huweza kuathiri mafigo na ini kusababisha kuharibika kwa utendaji. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 124.5°C Kiwango myeyuko: 12.6°C Uzito wiani: 0.99 g/cm³ Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 13°C: 12 Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 1 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.5 |
Kiwango cha kumweka: 24°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 235°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.3-17.0 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.67 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||