MAGNESIUM NITRATE ICSC: 1041
Mei 2003

Nitric acid, magnesium salt
CAS # 10377-60-3 Mg(NO3)2
RTECS # Masi ya molekuli: 148.33
UN # 1474
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usigusishe na vinavyoweza kuwaka na vinakisishaji.
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na vinakisishaji.


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi

Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Kuchanganyikiwa. Degedege. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kupoteza fahamu.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo vya plastiki. Osha salio kwa maji mengi.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 5.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 51GO2-I+II+III
Msimbo wa NFPA: H 2; F 0; R 3;
Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi. Kavu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
MAGNESIUM NITRATE ICSC: 1041
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE RISHAI ISO RANGI AU NYEUPE

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii ni kioksidishaji madhubuti na humenyuka iwapo na maunzi yanayoweza kuwaka na yanayonakisi kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki. MAK haijathibitishwa.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Kikolezo cha chembechembe yenye kusumbua yaweza kufikiwa haraka ikitawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Yaweza kusababisha muwasho wa mekaniko. Ikimezwa dutu hii huweza kuathiri damu kusababisha kufanyika kwa methemoglobini. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Hutengana chini ya kiwango mchemko ifikapo 330°C
Umumunyifu katika maji: vizuri sana
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi. Mapendekezo kwenye kadi hii pia yanahusu Magnesium nitrate hexahydrate (CAS 13446-18-9) ambayo inauzwa.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005