AMMONIUM OXALATE ICSC: 1036
Machi 1995

Oxalic acid, diammonium salt
Ethanedioic acid, diammonium salt
CAS # 1113-38-8 C2H8N2O4 / NH4OOCCOONH4
RTECS # RO2750000 Masi ya molekuli: 124.1
UN # 2811
EC # 607-007-00-3
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo. (Tazama Kumeza).
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi Wekundu. Mchomo. Maumivu. Malengelenge.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Degedege. Kusinzia. Mazimbwezimbwe. Mshtuko au kuzimia. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: Xn
R: 21/22
S: (2-)-24/25
Angalia: [A]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G12c
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho, vioksidishaji. Kavu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
AMMONIUM OXALATE ICSC: 1036
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA FUWELE ISO RANGI, ISO HARUFU

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa au inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi kama vile amonia na oksidi za nitrojeni. Humenyuka pamoja na vioksidishaji.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaokera unaweza kufikiwa haraka.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva na mafigo kusababisha kuharibika kwa utendaji.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri mafigo.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Hutengana chini ya kiwango myeyuko ifikapo - tazama Vidokezo
Uzito wiani (maji = 1): 1.50
Umumunyifu katika maji: wastani
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Maumbile ya asili ni yale ya monohidrati. Jotoridi linalosababisha mtengano haijulikani katika maandiko.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005