| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto.
|
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 65°C.
|
Mfumo funge wa zaidi ya 65°C, uingizaji hewa.
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Mchomo. Kikohozi. Kuumwa koo. Kukosa pumzi. Kupumua kwa shida. Kufanyiza kisauti wakati wa kupumua.
|
Zuia kuvuta hewa ya vumbi. Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Mibabuko ya ngozi. Maumivu. Malengelenge.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Mchomo. Maumivu ya tumbo. Kichefuchefu. Kutapika. Kuumwa kichwa. Udhaifu. Degedege. Mshtuko au kuzimia.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Uingizaji hewa. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vilivyofunikwa; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
|
Ainisho ya EU Alama: C R: 34-42/43-52/53 S: (1/2-)-22-26-36/37/39-45-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 8 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 80GC8-II+III Msimbo wa NFPA: H 3; F 2; R 1; |
Kinachotenganishwa na asidi kali, vioksidishaji vikali, anhidridi za asidi, vyakula na malisho, metali. Kavu. Kilichofungwa vizuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: FUWELE RISHAI ISO RANGI AU MAGAMBA NYEUPE YENYE HARUFU KALI. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapochomwa kuzalisha gesi zenye sumu na babuzi, kama vile oksidi za nitrojeni. Mmumunyo huu katika maji ni besi kali ya kati. Humenyuka pamoja na anhidridi asidi, asidi kali na vioksidishaji vikali, kusababisha athari ya moto. Hushambulia metali nyingi na kutoa gesi inayoweza kuwaka/lipukaji (Hidrojeni - tazama ICSC 0001). VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): MAK: Sah; (DFG 2002). Ona Vidokezo. |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Kuvuta pumzi kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Imemeswa kwa wingi dutu hii huweza kuathiri mfumo wa neva kusababisha kuharibika kwa utendaji na kupoteza fahamu. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Kuvuta hewa kwa kurudia au muda mrefu huweza kusababisha pumu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 146°C Kiwango myeyuko: 106°C Uzito wiani: 1.1 g/cm³ Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 15 Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 21 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1 Kiwango cha kumweka: 65°C Jotoridi la kujiwasha: 320°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 4-14 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -1.17 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa samaki.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Mtu yeyote aliyeonyesha dalili za pumu kutokana na dutu hii kamwe asigusane na dutu hiyo tena. Aghalabu dalili za pumu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Kwa hiyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Thamani ya MAK bado haijapatikana lakini hati kamili ipo (MAK IIb).
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||