PERACETIC ACID (stabilized) ICSC: 1031
Oktoba 2000

Peroxyacetic acid
Ethaneperoxoic acid
Acetyl hydroperoxide
CAS # 79-21-0 C2H4O3 / CH3COOOH
RTECS # SD8750000 Masi ya molekuli: 76.1
UN # 3105
EC # 607-094-00-8
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua. Kilipukaji.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na dutu ziwakazo. Usigusishe na nyuso za moto.
Mnyunyizio wa maji.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 40.5°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 40.5°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka. USIACHE kikaathiriwa na msuguano au mshtuko.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi. Kuumwa koo. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu. Tazama Vidokezo.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Maumivu. Malengelenge. Mibabuko ya ngozi.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Mchomo. Mshtuko au kuzimia.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vyenye plastiki vyenye mifuniko. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia). Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.

Ainisho ya EU
Alama: O, C, N
R: 7-10-20/21/22-35-50
S: (1/2-)-3/7-14-36/37/39-45-61
Angalia: [B, D]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 5.2
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 52G01b
Msimbo wa NFPA: H 3; F 2; R 4; ox
Isodhurika kwa moto. Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi, maunzi yasiokubaliana. Tazama Hatari za Kikemikali. Baridi. Hifadhi iwapo tu imetulia.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
PERACETIC ACID (stabilized) ICSC: 1031
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Huweza kutengana kwa mlipuko kutokana na mshtuko, msuguano, mtikiso. Huweza kulipuka wakati wa kukanza. Dutu hii ni kioksidishaji madhubuti na humenyuka kwa ukali sana iwapo na maunzi yanayoweza kuwaka na yanayonakisi. Dutu hii ni asidi dhaifu. Hushambulia metali mingi ikijumuisha alumini.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki. MAK haijathibitishwa.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Kuvuta pumzi kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo).

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 105°C
Kiwango myeyuko: 0°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.2
Umumunyifu katika maji: kuchanganyika
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 2.6
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.6
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.04
Kiwango cha kumweka: 40.5°C o.c.
Jotoridi la kujiwasha: 200°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: tazama Vidokezo
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Peracetic acid is always sold in solution with acetic acid and hydrogen peroxide. Vikomo vya ulipukaji havijulikani katika maandiko, japokuwa dutu hii inaweza kuwaka na ina kiwango cha kumweka pungufu ya 61°C. Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Ongezeko la kiimarishaji au kiviza huweza kuathiri tabia ya kitoksini za dutu hii, shauriana na mtaalam.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005