ETHYL ACETOACETATE ICSC: 1024
Aprili 2000

Acetoacetic acid ethyl ester
Ethyl acetylacetate
3-Oxobutanoic acid ethyl ester
1-Ethoxybutane-1,3-dione
CAS # 141-97-9 C6H10O3 / CH3COCH2COOC2H5
RTECS # AK5250000 Masi ya molekuli: 130.14
UN #
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 70°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 70°C, uingizaji hewa.

MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Kupumzika.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Osha salio kwa maji mengi.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Msimbo wa NFPA : H 2; F 2; R 0;
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Uingizaji hewa kwenye sakafu. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ETHYL ACETOACETATE ICSC: 1024
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vikali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki
MAK haifahamiki
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru hautafikiwa au utafikiwa polepole sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C wakati wa kunyunyiza au kutawanya, hata hivyo, kwa kasi zaidi.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 180.8°C
Kiwango myeyuko: -45°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.021
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 2.86
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.1
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.48
Kiwango cha kumweka: 70°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 295°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1-54
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.27
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO

MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005