ENDRIN ICSC: 1023
Oktoba 2000

CAS # 72-20-8 C12H8Cl6O
RTECS # IO1575000 Masi ya molekuli: 380.9
UN # 2761
EC # 602-051-00-X
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Michanganyiko ya vioevu vyenye vimumunyisho vya kaboni huweza kuwaka (moto). Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi (Tazama Kumeza).
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! (Tazama Kumeza).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Kizunguzungu. Udhaifu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kutapika. Degedege.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi kikali cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T+, N
R: 24-28-50/53
S: (1/2-)-22-36/37-45-60-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G41a
Msimbo wa NFPA: H 3; F 0; R ; 0
Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ENDRIN ICSC: 1023
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE NYEUPE

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa zaidi ya 245°C huzalisha kloridi hidrojeni, fosjini.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.1 mg/m³ (ngozi) (ACGIH 2000)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka wakati wa kunyunyiza au inapotawanywa hasa iwapo katika hali ya poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva kusababisha degedege na kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Hutengana chini ya kiwango mchemko ifikapo 245°C
Kiwango myeyuko: 200°C
Uzito wiani: 1.7 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: hakuna
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 25°C: sio na maana
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 5.34
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa nyuki, ndege na mamalia. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira. Kuzidisha kwa kemikali yaweza kutokeakwa samaki na kwa vyakula vya mgini. Dutu hii huingia katika mazingira kwa matumizi ya kawaida. Utaratibu wa hali ya juu lazima unahitajika ili kuzuia kiasi zaidi kisitokee kama kupitia kwa kutupwa ovyo.
VIDOKEZO
Angalia pia kadi ya viyeyusho endapo vimetumiwa kutengenezea dutu hii. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005