DIETHYL CARBONATE ICSC: 1022
Oktoba 2000

Carbonic acid diethyl ester
Ethyl carbonate
CAS # 105-58-8 C5H10O3 / (C2H5O)2CO
RTECS # FF9800000 Masi ya molekuli: 118.13
UN # 2366
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na strong vioksidishaji.
AFFF, povu linalokinza alkoholi, poda kavu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 25°C. Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na vioksidishaji vikali.
Mfumo funge wa zaidi ya 25°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kichefuchefu. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi
Glavu za kinga.
Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Kupumzika.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni).
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30G35
Msimbo wa NFPA: H 2; F 3; R 1;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Baridi. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
DIETHYL CARBONATE ICSC: 1022
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia plastiki na resini mingi.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki. MAK haijathibitishwa.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka wakati wa kunyunyiza.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho na njia ya upumuaji.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 126°C
Kiwango myeyuko: -43°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.98
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 1.1
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.07
Kiwango cha kumweka: 25°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 445°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.4-11.0
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Madhara kwa mazingira ya mkabala na dutu hii hayajachunguzwa vya kutosha.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005