CAMPHOR ICSC: 1021
Mei 2003

2-Bornanone
2-Camphanone
1,7,7-Trimethylbicyclo(2.2.1)heptan-2-one
CAS # 76-22-2 C10H16O
RTECS # EX1225000 Masi ya molekuli: 152.3
UN # 2717
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 66°C. Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
Mfumo funge wa zaidi ya 66°C, uingizaji hewa. Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.

MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo. Zaidi (tazama Kumeza).
Uingizaji hewa (hapana kama ni poda), mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwani ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Mchomo kooni na kifuani. Kichefuchefu. Kutapika. Kuhara. Kuumwa kichwa. Kuchanganyikiwa. Degedege. Kupoteza fahamu.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vilivyofunikwa; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio A/P2 cha mvuke kikaboni na vumbi linalodhuru.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 4.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 41GF1-II+III
Msimbo wa NFPA: H 0; F 2; R 0;
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, vinakisishaji vikali, vimumunyishaji venye klorini, vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
CAMPHOR ICSC: 1021
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE ISO RANGI AU NYEUPE YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa kuzalisha gesi zenye sumu and mafusho yakerayo. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali, kinakisishaji kikali na kiyeyusho chenye klorini, kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 2 ppm kama TWA; A4;
TLV: 3 ppm kama STEL; (ACGIH 2003).
MAK: 2 ppm, 13 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: II(2); (DFG 2002).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii kwenye joto la kawaida.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva kusababisha degedege na kusababisha matatizo ya kupumua. Ikimezwa mfiduo huweza kusababisha kifo.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 204°C
Kiwango myeyuko: 180°C, dutu hii hugeuka kuwa mvuke katika joto la nyumbani
Uzito wiani: 0.99 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 0.12
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 27
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 5.24
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1
Kiwango cha kumweka: 66°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 466°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 0.6-3.5
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Kafuri inapatikana katika isoma mbili (CAS 464-48-2 na 464-49-3) na kama mchanganyiko (racemic mixture) (CAS 21368-68-3).
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005