| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua sana. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na dutu ziwakazo. Usigusishe na uchafu. Usigusishe na nyuso za moto.
|
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
|
| MFIDUO |
|
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kukosa pumzi. Kuumwa koo.
|
Uingizaji hewa.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
|
Glavu za kinga.
|
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Miwani ya usalama.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Msokoto wa tumbo. Kutapika. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni).
|
Maunzi maalum. Ainisho ya EU Alama: O, F R: 7-11 S: (2-)-3/7-14-16-36/37/39 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 5.2 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 52G01. Msimbo wa NFPA: H 3; F 2; R 4; ox |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi. Baridi. Kilichofungwa vizuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI HADI MANJANO CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa ifikapo 111°C, ambayo huongeza athari ya moto. Dutu hii ni kioksidishaji madhubuti na humenyuka kwa ukali sana iwapo na maunzi yanayoweza kuwaka na yanayonakisi. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki. |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho na njia ya upumuaji. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko (hutengana): 111°C Kiwango myeyuko: -40°C Uzito wiani (maji = 1): 0.8 Umumunyifu katika maji: hakuna Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 2.6 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 5 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.1 Kiwango cha kumweka: 12°C c.c. Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1-4 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Vikomo vya ulipukaji havijulikani katika maandiko, japokuwa dutu hii inaweza kuwaka na ina kiwango cha kumweka pungufu ya 61°C. Madhara ya afya yatokanayo na kuingia mwilini dutu hii hayajachunguzwa vya kutosha. Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||