ANILINE HYDROCHLORIDE ICSC: 1013
Machi 2001

Benzenamine hydrochloride
Anilinium chloride
Aniline salt
CAS # 142-04-1 C6H8ClN / C6H7N . HCl
RTECS # CY0875000 Masi ya molekuli: 129.59
UN # 1548
EC # 612-009-00-2
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto. Usigusishe na vioksidishaji.
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na vioksidishaji.


MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo. Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Kuchanganyikiwa. Degedege. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kupoteza fahamu.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu. Tazama Vidokezo.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari. Tazama Vidokezo.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio A/P2 cha mvuke kikaboni na vumbi linalodhuru. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 20/21/22-40-48/23/24/25-50
S: (1/2-)-28-36/37-45-61
Angalia: [A]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G12c
Msimbo wa NFPA : H 3; F 1; R 0;
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi kali, vyakula na malisho. Kavu. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ANILINE HYDROCHLORIDE ICSC: 1013
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE NYEUPE KAMA RISHAI, HUGEUKA GIZA INAPOFIDULIWA NA HEWA NA MWANGA.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa au inapogusana na asidi huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi kama vile anilini, oksidi za nitrojeni na kloridi hidrojeni. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (kama anilini na misombo inayohusiana): 2 ppm; ngozi, A3 (ACGIH 2000).
Ainisho ya MAK 3b, ngozi (2000)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri damu, kusababisha kufanyika kwa methemoglobini. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kusababisha kifo. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Athari zinaweza kuchelewa. Tazama Vidokezo.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri damu, kusababisha kufanyika kwa methemoglobini.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 245°C
Kiwango myeyuko: 196-202°C
Uzito wiani: 1.22 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 107
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.46
Kiwango cha kumweka: 193°C o.c.
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Pia shauriana na ICSC 0011 Anilini.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005