| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua sana. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka. Ukanzaji unaweza kusababisha ongezeko la kanieneo na kuleta athari ya kupasuka.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Mnyunyizio wa maji, povu linalokinza alkoholi.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
|
| MFIDUO |
|
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Kuchanganyikiwa. Degedege. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kutokwa jasho. Kichefuchefu. Kupoteza fahamu. Kutapika. Kujisikia joto na kujaa usoni. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA!
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
|
Miwani ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
(Tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
|
Kisichoingiza hewa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 3 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30G30 Msimbo wa NFPA: H 1; F ; R 2; |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Baridi. Kilichofungwa vizuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU MANJANO CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. HATARI ZA KIKEMIKALI: Huweza kulipuka wakati wa kukanza. Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha gesi zenye sumu kama vile oksidi za nitrojeni. Humenyuka pamoja na vioksidishaji kusababisha athari ya moto na mlipuko. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki. |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kupitia katika ngozi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii huweza kuathiri damu na mfumo wa moyo na mishipakusababisha ugonjwa wa moyo na kufanyika kwa methemoglobini. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 97-99°C Uzito wiani (maji = 1): 0.875 Umumunyifu katika maji: hakuna Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 3.5 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.0 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.1 Kiwango cha kumweka: 3°C Jotoridi la kujiwasha: 209°C | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Mwako katika nafasi funge huenda ukageuka kuwa mpasuko. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||