PHOSPHORIC ACID ICSC: 1008
Oktoba 2000

Orthophosphoric acid
CAS # 7664-38-2 H3O4P / H3PO4
RTECS # TB6300000 Masi ya molekuli: 98.0
UN # 1805
EC # 015-011-00-6
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni. Tazama Vidokezo.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!

Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kukosa pumzi. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu. Mibabuko ya ngozi. Malengelenge.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Maumivu. Wekundu. Kuungua kunakopenya sana.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Mchomo. Mshtuko au kuzimia.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vilivyofunikwa; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: C
R: 34
S: (1/2-)-26-45
Angalia: [B]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 8
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 80G01
Msimbo wa NFPA : H 2; F 0; R 0;
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Tazama Hatari za Kikemikali. Kilichofungwa vizuri. Kavu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
PHOSPHORIC ACID ICSC: 1008
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE RISHAI, ISO RANGI

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hupolimisha kwa ukali sana kwa kuathiriwa na misombo ya azo na epoksidi. Inapowaka hutengeneza mafusho yenye sumu (oksidi za fosforasi). Dutu hii hutengana inapogusana na alkoholi, aldehidi, sianidi, ketoni, fenoli, esta, sulfidi, vikaboni vya kihalojeni huzalisha mafusho yenye sumu. Hushambulia metali nyingi na kutoa gesi inayoweza kuwaka/lipukaji (Hidrojeni - tazama ICSC 0001). Dutu hii ni asidi kali ya kati. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na besi.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 1 mg/m³ (ACGIH 1999).
TLV (as STEL): 3 mg/m³ (ACGIH 1999).
1 mg/m³ (8h), 2 mg/m³ (muda mfupi) EC OEL
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru hautafikiwa au utafikiwa polepole sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Hutengana chini ya kiwango mchemko ifikapo 213°C
Kiwango myeyuko: 42°C
Uzito wiani: 1.9 g/cm³
Umumunyifu katika maji: vizuri sana
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 4
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
KAMWE usimiminie maji dutu hii; wakati wa kumumunyisha au kuzimua, daima itie polepole kwenye maji.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005