LEAD DIOXIDE ICSC: 1001
Oktoba 2001

Lead peroxide
Lead(IV) oxide
CAS # 1309-60-0 PbO2
RTECS # OGO700000 Masi ya molekuli: 239.2
UN # 1872
EC # 082-001-00-6
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usigusishe na dutu ziwakazo. Usigusishe na vinakisishaji.
Moto unapotokea katika eneo: mnyunyizio wa maji.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na dutu za kuwaka na vinakisishaji.


MFIDUO
EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!

Kuvuta pumzi
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 61-20/22-33-50/53-62
S: 53-45-60-61
Angalia: [A, E]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 5.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 51S1872
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho na maunzi yasiokubaliana. Tazama Hatari za Kikemikali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
LEAD DIOXIDE ICSC: 1001
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE AU PODA KAHAWIA

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa ifikapo 290°C huzalisha oksijeni na mafusho yenye sumu. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na dutu zinazoweza kuwaka, vikaboni, sulfuri, peroksidi hidrojeni na fosforasi, kusababisha athari ya moto.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: kama Pb 0.05 mg/m³ A3 (ACGIH 2001).
MAK: kama Pb 0.05 mg/m³ (DFG 2000).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa hasa iwapo katika hali ya poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri damu, uboho, mfumo mkuu wa neva, mfumo wa neva wa pembeni na mafigo kusababisha anemia, athari kwa ubongo (kama kifafa), ugonjwa wa neva wa pembeni, tumbo kuuma na kuharibika kwa figo. Husababisha kusumisha kwa uzazi na kukua kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko (hutengana): 290°C
Uzito wiani: 9.38 g/cm³
Umumunyifu katika maji: hakuna
DATA YA MAZINGIRA
Kuzidisha kwa kemikali yaweza kutokea kwa mimea na kwa mamalia. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005