LEAD CARBONATE ICSC: 0999
Machi 2001

Carbonic acid, lead(2+) salt
Lead(2+) carbonate
Cerussite
CAS # 598-63-0 PbCO3
RTECS # OF9275000 Masi ya molekuli: 267.2
UN #
EC # 082-001-00-6
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 61-20/22-33-50/53-62
S: 53-45-60-61
Angalia: [A, E]
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G64c
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho and maunzi yasiokubaliana. Tazama Hatari za Kikemikali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
LEAD CARBONATE ICSC: 0999
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE ISO RANGI

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa ifikapo 315°C huzalisha mafusho yenye sumu (oksidi risasi). Humenyuka kwa ukali sana pamoja na florini, kusababisha athari ya moto.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (kama Pb): 0.05 mg/m³ A3 (ACGIH 2000).
MAK: 0.1 mg/m³; kama Pb (2000).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa hasa iwapo katika hali ya poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri damu, uboho, mfumo mkuu wa neva, mfumo wa neva wa pembeni na mafigo, kusababisha anemia, kupasuka kwa chembe ya damu, athari kwa ubongo (kama kifafa), ugonjwa wa neva wa pembeni, kuharibika kwa figo. Husababisha sumu kali inayoathiri uzazi kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko (hutengana): 315°C
Uzito wiani: 6.6 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml: 0.0001
DATA YA MAZINGIRA
Katika mfuatano wa ulishano ambao ni muhimu kwa binadamu, mlimbikizo wa kibiliolojia hutokea, hasa kwenye mimea na mamalia. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira kwa sababu hubakia kwenye mazingira.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005