| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki.
|
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kuumwa koo.
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu.
|
Miwanivuli ya usalama.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kutapika. Ladha ya metali.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu). Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu.
|
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi kikali cha maji/bahari. Ainisho ya EU Alama: Xn, N R: 22-36/37/38-50/53 S: (2-)-13-24/25-46-60-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 9 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 90G02
|
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Weka gizani.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: PODA FUWELE NYEUPE HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana polepole inapoathiriwa na mwanga huzalisha kloridi zebaki na zebaki. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV (kama Hg): 0.025 mg/m³ (ngozi) A4 (ACGIH 1999). MAK kama Hg: 0.1 mg/m³; BAT 25 ug/l katika damu; 100 ug/l katika makojoo (1999) MAK kama Hg STEL: 1 mg/m³; (1999) Ainisho ya MAK Sh (1999) |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, mafigo na mfumo wa neva wa pembeni, kusababisha kutotembea vizuri, mvuruko wa fahamu na akili, uchovu, ulegevu wa misuli na kuharibika kwa figo. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango usablimishaji: 400-500°C Uzito wiani: 7.15 g/cm³ Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: hakuna |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira kwa sababu hubakia kwenye mazingira. Epusha kuingia katika mazingira tofauti na matumizi ya kawaida.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Usichukue nguo za kazi nyumbani. Cyclosan, M-C Turf fungicide ni majina ya kibiashara. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||