MERCURIC OXIDE ICSC: 0981
Machi 2001

Mercury (II) oxide
CAS # 21908-53-2 HgO
RTECS # OW8750000 Masi ya molekuli: 216.6
UN # 1641
EC # 080-002-00-6
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usigusishe na vinakisishaji.
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kikohozi.
Epuka kuvuta pumzi yenye vumbi laini au ukungu. Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu.
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzikikali cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T+, N
R: 26/27/28-33-50/53
S: (1/2-)-13-28-45-60-61
Angalia: [A]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G64b
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho, vinakisishaji, klorini na dutu tendaji nyingine. Tazama Hatari za Kikemikali. Weka gizani.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
MERCURIC OXIDE ICSC: 0981
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA FUWELE NZITO, MANJANO AU RANGI YA MACHUNGWA-MANJANO AU NYEKUNDU,

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana kwa kuathiriwa na mwanga na inapokanzwa zaidi ya 500°C huzalisha mafusho yenye sumu sana ya zebaki na oksijeni, ambayo huongeza athari ya moto. Humenyuka vikali pamoja na kinakisishaji, klorini, peroksidi hidrojeni, magnesiamu (katika joto), dikloridi disulfuri na trisalfidi hidrojeni. Misombo isiyohimili mshtuko hutengenezwa kwa metali na vitu kama vile sulfuri na fosforasi.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (kama Hg): 0.025 mg/m³ A4 (ngozi) (ACGIH 2000).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri mafigo, kusababisha kuharibika kwa figo.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko (hutengana): 500°C
Uzito wiani: 11.1 g/cm³
Umumunyifu katika maji: hakuna
DATA YA MAZINGIRA
Katika mfuatano wa ulishano ambao ni muhimu kwa binadamu, mlimbikizo wa kibiliolojia hutokea, hasa kwenye viumbe hai vya majini. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira kwa sababu hubakia kwenye mazingira.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Red na Yellow mercuric oxide ni majina ya kawaida.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005