FENCHLORPHOS ICSC: 0975
Oktoba 1995

O,O-Dimethyl-O-(2,4,5-trichlorophenyl) phosphorothioate
Ronnel
CAS # 299-84-3 (CH3O)2PSOC6H2Cl3 / C8H8Cl3O3PS
RTECS # TG0525000 Masi ya molekuli: 321.5
UN #
EC # 015-052-00-X
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Michanganyiko ya vioevu vyenye vimumunyisho vya kaboni huweza kuwaka (moto). Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)! EPUKA MFIDUO KWA VIJANA NA WATOTO!

Kuvuta pumzi Kizunguzungu. Kutokwa jasho. Kupumua kwa shida. Kupoteza fahamu. Kutapika. Msongo/mfinyo (wa jicho), kukakamaa kwa msuli, utokaji mate kwa wingi.
Epuka kuvuta pumzi yenye vumbi laini au ukungu. Uingizaji hewa (hapana kama ni poda), mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA!
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Msokoto wa tumbo. Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika. Msongo/mfinyo (wa jicho), kukakamaa kwa msuli, utokaji mate kwa wingi.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: Xn
R: 21/22
S: (2-)-25-36/37
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, vyakula na malisho.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
FENCHLORPHOS ICSC: 0975
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA NYEUPE

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu kama vile kloridi hidrojeni, oksidi za fosforasi na oksidi za sulfuri.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 10 mg/m³ (kama TWA) (ACGIH 1995-1996)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaokera unaweza kufikiwa haraka kwa kunyunyiza au kutawanywa hasa kama poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa nevakusababisha degedege. Kizuizi cha kolinesterasi. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii inaweza kusababisha ulemavu kwa watoto wa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 41°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.48
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: hakuna
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 25°C: <10
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 4.88
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Kuzidisha kwa kemikali yaweza kutokea kwa samaki. Dutu hii huingia katika mazingira kwa matumizi ya kawaida. Utaratibu wa hali ya juu lazima unahitajika ili kuzuia kiasi zaidi kisitokee kama kupitia kwa kutupwa ovyo.
VIDOKEZO
Jotoridi linalosababisha mtengano haijulikani katika maandiko. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Ectoral, Trolene, Viozene, Nankor na Korlan ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005