BROMINE PENTAFLUORIDE ICSC: 0974
Aprili 2000

Bromine fluoride
CAS # 7789-30-2 BrF5
RTECS # EF9350000 Masi ya molekuli: 174.9
UN # 1745
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usigusishe na dutu ziwakazo. Usigusishe na maji, vitu vikaboni na vinavyoweza kuwaka.
Moto unapotokea katika eneo: tumia dioksidi kaboni mchanga mkavu au poda. USITUMIE vitenzi vyenye maji.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na maji au mvuke, fueli na vikaboni.

Utokeapo moto: poza mapipa n.k. kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kukosa pumzi. Kuumwa koo. Kupumua kwa shida. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Mfumo funge na uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu. Mibabuko ya ngozi. Malengelenge.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vaa glavu za kinga unapotoa huduma ya kwanza. Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kiwaa. Kuungua kunakopenya sana.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Mchomo. Mshtuko au kuzimia.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia iliyobaki kwa vermikuliti au udongo kavu au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Kisichoingiza hewa. Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 5.1
Jasara tanzu za UN: 6.1 na 8
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 51G11
Msimbo wa NFPA : H 4; F 0; R 3; W; OX
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho na dutu zote. Tazama Hatari za Kikemikali. Kavu. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
BROMINE PENTAFLUORIDE ICSC: 0974
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU MANJANO ISIYOKOZA HADI KISICHO RANGI, KIFUKACHO, CHENYE HARUFU KALI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa zaidi ya 460°C na inapogusana na asidi au mafusho ya asidi huzalisha mafusho yenye sumu sana, floridi hidrojeni (tazama ICSC 0283) na bromidi hidrojeni (tazama ICSC 0282). Humenyuka kwa ukali ikiwa na fueli na misombo kikaboni, dutu zenye hidrojeni (mfano amonia, asidi asetiki, grisi, karatasi), kusababisha athari ya moto na mlipuko. Humenyuka kwa mlipuko pamoja na maji au mvuke kutoa mafusho yenye sumu na babuzi, floridi hidrojeni na bromidi hidrojeni. Huadhiri na elementi zote lakini sio na nitrojeni, oksijeni na gesi hadimu.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.1 ppm; 0.72 mg/m³ (ACGIH 1999)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Kuvuta pumzi ya mvuke wake kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Mfiduo huweza kusababisha kifo.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii husababisha mabadiliko kwa mifupa kwa sababu ya florini (fluorosis), kufanyisha floridi hidrojeni, zaidi tazama ICSC 0283 floridi hidrojeni.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 41°C
Kiwango myeyuko: -61°C
Uzito wiani (maji = 1): 2.5
Umumunyifu katika maji: mmenyuko
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 44
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 6.1
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Humenyuka kwa nguvu na vitenzi vya kuzimia moto kama vile maji. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005