alpha-NAPHTHYLTHIOUREA ICSC: 0973
Aprili 2000

Antu
1-(1-Naphthyl)-2-thiourea
1-Naphtylthiourea
CAS # 86-88-4 C11H10N2S / C10H7NHCSNH2
RTECS # YT9275000 Masi ya molekuli: 202.3
UN # 1651
EC # 006-008-00-0
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka katika hali mahususi. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA!
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho
Miwanivuli ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kutapika. Kupumua kwa shida.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T+
R: 28-40
S: (1/2-)-25-36/37-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G12b
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, nitrati silva, vyakula na malisho.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
alpha-NAPHTHYLTHIOUREA ICSC: 0973
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA FUWELE NYEUPE ISO HARUFU

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha gesi zenye sumu na mafusho yenye sumu kama vile oksidi za nitrojeni, oksidi za sulfuri na monoksidi kaboni. Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vikali kama vile nitrati silva. kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (kama TWA): ppm; 0.3 mg/m³ A4 (ACGIH 1999).
MAK: ppm; 0.3 mg/m³; kama I (1999)
Ainisho ya MAK II.2 (1999)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Mfiduo kwa dutu hii huweza kusababisha uvimbe wa mapafu. Kuvuta pumzi kunaweza kusababisha (tazama Vidokezo). Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Hutengana kabla ya kuchemka: tazama Vidokezo
Kiwango myeyuko: 198°C
Uzito wiani: >1 g/cm³
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 25°C: 0
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 7.0
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.66 (imekadiriwa)
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Taka za kawaida zilizopo zinaweza kubadili tabia za kitoksini za dutu hii; mwoone mtaalam kwa ushauri. Zoa la kitekinikali ni poda bluu-kijivu. Jotoridi linalosababisha mtengano haijulikani katika maandiko. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Anturate, Bantu, Kill Kantz, Krysid, Rattrack na Rat-tu ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005