| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto.
|
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Degedege. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kupoteza fahamu.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. (Tazama Kuvuta pumzi).
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
|
| Macho |
|
Kingao cha uso.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. (Tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari. Ainisho ya EU Alama: T+, N R: 45-26/27/28-33-51/53 S: 53-45-61 Angalia: [E] Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 849 Msimbo wa NFPA : H 2; F 1; R 0; |
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi, anhidridi za asidi, kloridi za asidi, klorofometi, vyakula na malisho. Tazama Hatari za Kikemikali.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU NYEKUNDU HADI MANJANO KAMA MAFUTA, CHENYE HARUFU TAMBULISHI. , HUGEUKA KAHAWIA INAPOFIDULIWA NA HEWA. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu (oksidi za nitrojeni). Humenyuka pamoja na asidi, anhidridi za asidi, kloridi za asidi, klorofometi na vioksidishaji vikali. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 0.1 ppm (kama TWA) (A3) (ngozi) (ACGIH 1998). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C wakati wa kunyunyiza au kutawanya, hata hivyo, kwa kasi zaidi. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii huweza kuathiri damu, kusababisha kufanyika kwa methemoglobini. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Tazama Vidokezo. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 213°C Kiwango myeyuko: 5°C Uzito wiani (maji = 1): 1.1 Umumunyifu katika maji, g/100 ml: 1.5 Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 2 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.25 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.0 Kiwango cha kumweka: 118°C o.c. Jotoridi la kujiwasha: 415°C Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.18 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kusababisha madhara yatakayoonekana baadaye katika mazingira ya maji.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Pia shauriana na ICSC #0971 p-Anisidine.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||