2,4,6-TRINITROTOLUENE ICSC: 0967
Aprili 2000

2-Methyl-1,3,5-trinitrobenzene
1-Methyl-2,4,6-trinitrobenzene
TNT
CAS # 118-96-7 C7H5N3O6 / C6H2(CH3)(NO2)3
RTECS # XU0175000 Masi ya molekuli: 227.1
UN # 0209
EC # 609-008-00-4
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Kilipukaji. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Maji mengi. Usijaribu kuzima mioto mikubwa, ondoka katika eneo la hatari.
MLIPUKO Hatari ya moto na kulipuka hutokea ikipashwa joto haraka au ikipata mshituko mkubwa.
USIACHE kikaathiriwa na msuguano au mshtuko. Usipashe joto na weka kwa mnyevu wa maji usiozidi thelathini kwa mia.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kuumwa kichwa. Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Kikohozi. Kuumwa koo. Kupumua kwa shida. Kutapika. Msokoto wa tumbo. Kupoteza fahamu. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Maumivu. Madoa ya manjano kwenye ngozi. (Tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu. Vaa glavu za kinga unapotoa huduma ya kwanza.
Macho Wekundu. Maumivu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Vaa glavu ukijaribu kusababisha kutabika.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Ikimwagika nyenzo hii isifagiliwe ikiwa kavu. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: E, T, N
R: 2-23/24/25-33-51/53
S: (1/2-)-35-45-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 1.1D

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 10G03
Msimbo wa NFPA : H 2; F 4; R 4;
Isodhurika kwa moto. Tenga mbali na yale inayoweza kuanzisha mlipuko, na vyakula na malisho, maunzi yasiokubaliana. Tazama Hatari za Kikemikali. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
2,4,6-TRINITROTOLUENE ICSC: 0967
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE ISO RANGI HADI MANJANO

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Huweza kutengana kwa mlipuko kutokana na mshtuko, msuguano, mtikiso. Ikikanzwa dutu hii hulipuka ifikapo 240°C. Inapokanzwa, hutoa mafusho yenye sumu. Humenyuka vikali ikiwa na kemikali nyingi (shauriana na mtaalam), kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.1 mg/m³ (ngozi) (ACGIH 1999).
MAK: 0.01 ppm; 0.09 mg/m³; ngozi (1999)
Ainisho ya MAK 3 (1999)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri damu, kusababisha hemolysis, kufanyika kwa methemoglobini. Mfiduo huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo). Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Dutu hii huweza kuathiri ini, damu na macho kusababisha homa ya manjano, mtoto wa macho na upungufu wa damu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko (hutengana): 240°C
Kiwango myeyuko: 80.1°C
Uzito wiani: 1.65 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.013
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: sio na maana
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 7.85
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.60
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kusababisha madhara yatakayoonekana baadaye katika mazingira ya maji. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira kwa sababu hubakia kwenye mazingira.
VIDOKEZO
Mwako katika nafasi funge huenda ukageuka kuwa mpasuko. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005