TRIMETHYLCHLOROSILANE ICSC: 0966
Machi 2002

Chlorotrimethylsilane
Trimethyl silyl chloride
Chlorotrimethylsilicane
CAS # 75-77-4 C3H9ClSi / (CH3)3SiCl
RTECS # VV2710000 Masi ya molekuli: 108.7
UN # 1298
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua sana. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na nyuso za moto.
AFFF, dioksidi kaboni, mchanga mkavu, poda maalum. USITUMIE vitenzi vya majimaji. USITUMIE maji.
MLIPUKO Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
Utokeapo moto: poza mapipa n.k. kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kuumwa koo. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu. Tazama Vidokezo.
Ngozi Wekundu. Maumivu. Malengelenge. Mibabuko ya ngozi.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Mchomo. Maumivu ya tumbo. Mshtuko au kuzimia.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Usimpe chochote cha kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vikavu vinavyozibika. Usitumie vyombo vya plastiki. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga mkavu au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Jasara tanzu za UN: 8
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30GFC-II-X
Msimbo wa NFPA: H 3; F 3; R 2; W
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na other compounds, vyakula na malisho. Baridi. Kavu. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
TRIMETHYLCHLOROSILANE ICSC: 0966
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU KALI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi kama vile kloridi hidrojeni, fosjini. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na maji kusababisha kloridi hidrojeni (tazama ICSC 0163). Humenyuka kwa ukali sana pamoja na alkoholi, amini kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia metali nyingi iwapo kuna maji.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii na mvuke huu husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Kuvuta pumzi ya mvuke wake kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Mfiduo huweza kusababisha kifo. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 57°C
Kiwango myeyuko: -58°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.85
Umumunyifu katika maji: mmenyuko
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 26.7
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.8
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.7
Kiwango cha kumweka: -27°C
Jotoridi la kujiwasha: 395°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.8-6
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Humenyuka kwa nguvu na vitenzi vya kuzimia moto kama vile maji. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Asili ya taaluma ya sumu ni kama methilidiklorosilini (ICSC0279).
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005