| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Hutoa moshi wenye sumu ukiwa motoni. Kilipukaji.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na nyuso za moto.
|
FIKIRIA KUTOKA. Maji yaweza kutumika kwa moto kidogo. Usijaribu kuzimia moto mkubwa.
|
| MLIPUKO |
Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani. Hatari ya moto na mlipuko ikipata mshindo au ikipata joto au mwale.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza). USIACHE kikaathiriwa na msuguano au mshtuko. Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Insomnia. Maumivu ya tumbo. Kikohozi. Kuhara. Kuumwa kichwa. Kuumwa koo. Kutokwa damu puani.
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu. Madoa ya manjano kwenye ngozi na nywele.
|
Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Vaa glavu za kinga unapotoa huduma ya kwanza.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Kichefuchefu. (Tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu).
|
Ainisho ya EU Alama: E, T R: 2-23/24/25-33 S: (1/2-)-35-45 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 1.1D | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
|
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Weka gizani. Weka kwa nyumba tofauti ikikingwa kutokana na shindo ikifungwa kabisa.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: FUWELE ISO RANGI HADI MANJANO, ISO HARUFU HATARI KWA MWILI: Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Huweza kutengana kwa mlipuko kutokana na mshtuko, msuguano, mtikiso. Dutu hii hutengana ipasukapo inapokanzwa hadi 187°C. Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vingine kusababisha athari ya moto na mlipuko. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: (kama TWA) 1.5 mg/m³ (ACGIH 1997) |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa ya erosoli. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa neva. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Kuvuta hewa kwa kurudia au muda mrefu huweza kusababisha pumu. Dutu hii huweza kuathiri ini, mafigo na damu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango myeyuko: 130°C Uzito wiani (maji = 1): 1.57 Umumunyifu katika maji: hakuna Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: <0.1 |
Kiwango cha kumweka: hupasuka kwa hewa ifikapo 187°C | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||