SULFUR MONOCHLORIDE ICSC: 0958
Aprili 1997

Sulfur chloride
Disulfur dichloride
Sulfur subchloride
CAS # 10025-67-9 Cl2S2
RTECS # WS4300000 Masi ya molekuli: 135.03
UN # 1828
EC # 016-012-00-4
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, dioksidi kaboni. USITUMIE vitenzi vya majimaji. USITUMIE maji.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza mapipa n.k. kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi Kuumwa koo. Kikohozi. Mchomo. Kukosa pumzi. Kupumua kwa shida. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Maumivu. Wekundu. Malengelenge. Mibabuko ya ngozi.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Maumivu. Wekundu. Kuungua kunakopenya sana. Upofu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Mchomo. Maumivu ya tumbo. Mshtuko au kuzimia.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Katisha kioevu kilichomwagika kwa uangalifu kwa majivu ya soda na chokaa. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: C
R: 14-34-37
S: (1/2-)-26-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 8
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 734
Msimbo wa NFPA: H 2; F 1; R 1;
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, peroksidi, oksidi za fosforasi, ambatani ya oganiki, vyakula na malisho. Baridi. Kavu. Kilichofungwa vizuri. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
SULFUR MONOCHLORIDE ICSC: 0958
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU MANJANO-NYEKUNDU, KAMA MAFUTA, KIFUKACHO CHENYE HARUFU KALI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa au inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi kama vile kloridi hidrojeni, sulfidi hidrojeni, oksidi za sulfuri. Humenyuka pamoja na peroksidi, oksidi za fosforasi na ambatani ya oganiki, kusababisha athari ya moto na mlipuko. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na maji kufanyiza sulfuri, kloridi hidrojeni, dioksidi sulfuri, sulfidi hidrojeni, sulfiti na thiosulfati. Hushambulia metali nyingi iwapo kuna maji.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (kama viwango vya juu kabisa): 1 ppm; 5.5 mg/m³ (ACGIH 1996)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Inayotoza machozi. Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Kuvuta pumzi ya mvuke wake kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 138°C
Kiwango myeyuko: -77°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.7
Umumunyifu katika maji: mmenyuko
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.90
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.7
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.03
Kiwango cha kumweka: 118.5°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 234°C
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Humenyuka kwa nguvu na vitenzi vya kuzimia moto kama vile maji. Kikomo thamani cha mfiduo matumizi ya kazi kisivukwe wakati wowote wa mfiduo amilifu. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005