ROTENONE ICSC: 0944
Aprili 2000

Tubotoxine
Derris powder
CAS # 83-79-4 C23H22O6
RTECS # DJ2800000 Masi ya molekuli: 394.45
UN # 2588
EC # 650-005-00-2
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizo wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MFIDUO KWA VIJANA NA WATOTO!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kuchanganyikiwa. Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kutetemeka. Kupumua kwa shida. Kichefuchefu. Kuumwa koo. Kupoteza fahamu.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga.
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Msokoto wa tumbo. Degedege. Kuhara. Kutapika. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo visiyopitisha hewa; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu). Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 25-36/37/38-50/53
S: (1/2-)-22-24/25-36-45-60-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G41c
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ROTENONE ICSC: 0944
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE ISO RANGI

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yanayokereketa.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: ppm; 5 mg/m³ (kama TWA) (ACGIH 1999).
MAK: ppm; 5 mg/m³; (sehemu pumuzi ya erosoli (1999)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, kusababisha degedege na upungufu katika kupumua.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mafigo na ini.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Hutengana kabla ya kuchemka
Kiwango myeyuko: 165-166°C
Uzito wiani: 1.27 g/cm³
Umumunyifu katika maji: hakuna
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 4.10
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Epusha kuingia katika mazingira tofauti na matumizi ya kawaida. Dutu hii inaweza kusababisha madhara yatakayoonekana baadaye katika mazingira ya maji.
VIDOKEZO
Dutu hii inaweza kuwaka lakini kiwango mlipuko hakikuelezwa katika maandiko. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005