PROPYLENEDIAMINE ICSC: 0942
Aprili 1997

1,2-Propanediamine
1,2-Diaminopropane
CAS # 78-90-0 C3H10N2
RTECS # TX6650000 Masi ya molekuli: 74.1
UN # 2258
EC # 612-100-00-7
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, povu linalokinza alkoholi, maji mengi, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 33°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 33°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kuumwa koo. Kikohozi. Mchomo. Kukosa pumzi. Kupumua kwa shida. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Maumivu. Wekundu. Malengelenge. Mibabuko ya ngozi.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Maumivu. Wekundu. Kuungua kunakopenya sana. Upofu.
Miwanivuli ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Mchomo. Msokoto wa tumbo. Mshtuko au kuzimia.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Ainisho ya EU
Alama: C
R: 10-21/22-35
S: (1/2-)-26-37/39-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 8
Jasara tanzu za UN: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Msimbo wa NFPA: H 2; F 3; R 0;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho, vioksidishaji vikali, asidi, anhidridi asidi, kloridi asidi. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
PROPYLENEDIAMINE ICSC: 0942
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, KIRISHAI CHENYE HARUFU KALI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa au inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu (oksidi za nitrojeni). Dutu hii ni besi kali humenyuka vikali ikiwa na asidi na husababisha ulikaji. Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vikali, anhidridi asidi, na kloridi asidi. Humenyuka na sabaki kufanyiza ambatani iliyoepesi kwa shindo kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
MAK haijathibitishwa.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi ya mvuke wake kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Kumeza kioevu hiki kunaweza kusababisha madhara kwenye mapafu kukifyonza na kunaweza kuleta kichomi kinachotokana na kemikali. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 117-121°C
Kiwango myeyuko: -17°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.9
Umumunyifu katika maji: humumunyika
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 1.0
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.6
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.02
Kiwango cha kumweka: 33°C o.c.
Jotoridi la kujiwasha: 416°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2.2-11.1
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -1.8
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Dalili za kuvimba kwa mapafu hazijitokezi mpaka saa chache au siku chache zimepita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Kwa hiyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005